ZINAZOVUMA:

WHO yaipongeza Tanzania

Shirika la Umoja wa Afya duniani WHO limeipongeza Tanzania kwa...

Share na:

Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Tedros Ghebreyesus ameipongeza Tanzania kwa juhudi inazoendelea kufizanya katika kupambana ya kudhibiti magonjwa ya mlipuko kuingia na kuenea nchini Tanzania.

Dk. Tendros amesema hayo kwenye kikao maalum na wajumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Marzui pamoja na viongozi wengine waandamizi wakiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk Seif Shekalaghe, Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Tumaini Nagu pamoja na wataalamu wengine katika sekta ya afya.

Dk Tedros ameipongeza Tanzania kwa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Marburg na kwa kushirikiana na WHO katika kuimarisha huduma za uchunguzi na udhibiti dhidi ya magonjwa ya mlipuko.

Tanzania imeungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa chini ya WHO kushiriki kikao hicho cha 76 cha Shirika la Afya Duniani kinachofanyika Geneva, Uswisi.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya