ZINAZOVUMA:

Waziri Silaa kuongoza kliniki ya Ardhi Tanga

Waziri Jerry Silaa wa Ardhi anategemewa kuongoza kliniki ya Ardhi...

Share na:

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi Jerry Silaa anatarajiwa kuongoza Kliniki ya Ardhi kwa mkoa wa Tanga itakayofanyika kuanzia Aprili 22 hadi 28 mwaka huu, ikifanyika kwenye maeneo mawili Kijiji cha Miaka 21 Chumbageni na Korogwe.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Tanga, Tumaini Gwakisa alisema zoezi hilo litafanyika kwenye maeneo mawili ambapo litaanzia Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Mkoa wa Tanga eneo la Kijiji cha miaka 21 Chumbageni kuanzia Aprili 22 mpaka 25 mwaka huu”.

Alisema baada ya kumalizika Tanga wataelekea wilayani Korogwe, ambapo litafanyika kuanzia Aprili 26 mpaka 28 mwaka hu na uendeshwaji wa program hiyo utasimaiwa na itaongozwa na Waziri wa Ardhi Jerry Silaa akiwa na wataalamu wa Wizara hiyo.

“Nichukue nafasi hii kuwaalika wananchi wote wa mkoa wa Tanga kuhudhuria na kupata huduma mbalimbali za sekta ya ardhi katika maeneo ambayo kliniki hiyo itafanyika kwani kutakuwa na utatuzi wa migogoro ya ardhi ambapo Waziri atasikiliza kero mbalimbali za Migogoro hiyo” Alisema.

Alisema pia kutakuwa na utolewaji wa elimu kuhusu usimamizi wa ardhi pamoja na uwepo wa kituo jumuishi kitakachotoa huduma ya kupokea maoni mbalimbali na utoaji hati miliki, ukadiriaji wa kodi ya ardhi na ulipaji wa kodi ya ardhi.

Gwakisa aliwataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuhudhuria na kushiriki ambapo Waziri atakuwepo na wataalamu kutoka Wizarani.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya