Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda, leo alisikiliza maelezo ya watu wawili juu ya mgogoro wa umiliki wa ardhi mtaa wa Changanyikeni kata ya Toangoma ambapo baada ya kusikiliza pande zote mbili ameahidi kutatua mgogoro huo Alhamis ijayo.
Eneo la Block 25 lilipimwa na Wizara ya ardhi kati ya mwaka 2006 na 2008 limezua sitofahamu kuhusu uhalali wa umiliki kati ya wakazi wa asili wa eneo hilo na watu waliouziwa ardhi na wizara.
Mkuu huyo wa wilaya ameahidi kurudi tena Alhamisi ya tarehe 21.03.2024 akiwa na orodha ya wananchi wote waliolipwa fidia na wizara pamoja na maafisa wa ardhi na mipango miji toka Wizarani na Halmashauri Manispaa ya Temeke.
DC Temeke yuko kwenye operesheni maalum ya kusikiliza kero za wananchi na kutatua migogoro ya ardhi wilaya ya Temeke, Kata kwa Kata, aliyoianza mwanzoni mwa mwaka huu.