ZINAZOVUMA:

Waziri Mkuu: “Kuweni kama kina Ali Kamwe”.

Waziri Mkuu awataka maafisa habari wa serikali kufuata nyayo za...

Share na:

Waziri Mkuu, Mhe. Kassimu Majaliwa amewataka maafisa habari wa serikali kuiga mfano jinsi maafisa habari waliopo kwenye michezo wanavyotoa taarifa zao.

Amezungumza na maafisa habari hao katika kikao kazi cha 18 cha maafisa habari, uhusiano na mawasiliano wa serikali katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es salaam leo Machi 27.

Waziri Mkuu amesema hayo akiwataka maafisa habari kuhakikisha wanatoa taarifa kwa muda sahihi kama wanavyofanya kina Ahmedi Ally, Ali Kamwe, Masau Bwire na kifaru.

Mifano hiyo ameitoa kwa maafisa habari wa serikali kuonesha uharaka wa maafisa habari wa michezo wanaokua nao katika kutoa taarifa za timu zao.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya