ZINAZOVUMA:

Waziri Mkuu aiombea kura Tanzania Baraza la michezo

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ameiombea kura Tanzania kuwa makao makuu...

Share na:

Baraza la michezo la umoja wa Afrika kanda IV limefanya mkutano leo Mei 4, 2023 jijini Arusha, uliowakutanisha wajumbe wa mkutano huo ambao ni mawaziri wa michezo wa nchi hizo 14.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa baraza hilo ambalo linaundwa na nchi 14 za Eritrea, Djibout, Ethiopia, Sudan, Kenya, Madagaska, Mauritania, Rwanda, Visiwa vya Shelisheli, Rwanda, Somalia, South Sudan, Uganda na Tanzania.

Waziri Mkuu ametumia nafasi hiyo kuwaomba mawaziri hao kuifikiria Tanzania na hatimaye kuipa kura ya ndiyo ili Tanzania ndiyo iwe Makao Makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Ukanda wa IV

Aidha Waziri Mkuu amesema tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kuleta mafanikio ya kimataifa katika ukanda huu na kuchukua ubingwa wa vikomba mbalimbali vya kimataifa.

“Tunataka kuona timu zetu zinashinda makombe ya Kimataifa hasa Kombe la Dunia. Sisi tunaweza tukiamua kuwekeza kwenye miundombinu ya michezo na ujuzi pamoja na kushirikiana kwa pamoja”.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya