Makumi ya waandamanaji nchini Kenya wamelazwa hospitalini wakiwa na majeraha ya risasi huku watu wengine watatu wakiripotiwa kufariki katika siku ya kwanza ya Jana ya maandamano ya siku tatu nchini humo.
Matukio ya kutisha yameshuhudiwa katika siku ya kwanza ambapo polisi wameripotiwa kutumia risasi kukabiliana na waandamanaji wanaopinga kupanda kwa gharama za maisha huku watu wengi wakijeruhiwa.
Wasimamizi wa haki za binadamu wamelaani kitendo cha polisi cha kutumia nguvu na kuwapiga risasi raia.
Upinzani unasema siku ya kwanza ya maandamano imekuwa ya mafanikio na kuwataka wafuasi wao kujitokeza hii leo tena katika mji wa Nairobi.
Kwa upande mwingine, mamlaka zinasema kuwa ni mikoa michache tu iliyoathiriwa na kutangaza kufunguliwa kwa shule huko Nairobi na Mombasa.