ZINAZOVUMA:

Watu nane wafariki baada ya jengo kuporomoka

Watu nane wamepoteza maisha na mmoja kujeruhiwa baada ya jengo...

Share na:

Watu nane wakiwemo saba kutoka katika familia moja wamefariki mjini Cairo, baada ya jengo walilokuwa wakiishi kuporomoka.

Taarifa kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka imesema jengo hilo lililopo katika wilaya ya Hadayek al-Oubba liliporomoka na kuua watu nane.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa wafanyakazi wa ulinzi na raia waliwaokoa watu tisa, miongoni mwao mwanamke aliyejeruhiwa, huku wengine nane wakiwa wamepoteza maisha.

Watu wengine watano walifanikiwa kuondoka kwenye jengo hilo kabla ya kuporomoka, taarifa hiyo imesema.

Taarifa ya ofisi ya mwendesha mashtaka imesema mwanamke aliyejuriwa na wakazi wengine wawili wametoa ushahidi wakieleza kuwa kuporomoka kwa jengo hilo kulisababishwa na mkazi ambaye alibomoa ukuta katika makazi yake kwenye ghorofa ya kwanza licha ya majirani kumtaka asifanye hivyo.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya