ZINAZOVUMA:

Wananchi wadai kusitishwa matumizi ya petroli U.S

Wananchi mjini New York wameandamana wakimtaka Raisi Joe Biden asitisha...

Share na:

Maelfu ya watu wamekusanyika mjini New York, Marekani kutoa wito wa kuongezwa juhudi za kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi, ikiwemo kusitisha matumizi ya Petroli.

Mkusanyiko huo umeitishwa na taasisi zaidi ya 700 na makundi ya wanaharakati ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Waandamanaji walikusanyika kwenye mitaa kadhaa ya mji wa New York yaliko Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wakati viongozi mbalimbali duniani wakiwasili kuhudhuria mkutano huo utakaoanza siku ya Jumanne Septemba 19.

Waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kama vile “Biden, komesha matumizi ya nishati za petroli”.

Ujumbe kwenye mabango hayo ulikuwa unaakisi madhara ya mafuta ya petroli katika kuchafua mazingira na pia kukumbusha jinsi mabadiliko ya tabia ya nchi yanavyoongeza majanga ya asili kama moto na mafuriko duniani.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya