ZINAZOVUMA:

Wahitimu wa udaktari wafutiwa shahada zao.

St Augustine Tanzania imewafutia shahada wahitimu wa udaktari 162 kwa...

Share na:

Chuo cha St Augustine Tanzania kimefuta Shahada za udaktari Kwa wahitimu 162 waliohitimu Chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha mtakatifu Francis (SFUCHAS) kuanzia mwaka 2015 hadi 2019.

Sababu za kufuta Shahada hizo ni kugoma kwa madaktari hao kurejesha nyaraka za matokeo (transcript) ambazo walipewa bila Baraza la seneti la Chuo kuwa na taarifa na kuziidhinisha.

Uongozi wa SAUT kupitia mwenyekiti wa balaza la seneti la Chuo Prof. Costa Mahalu umeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao cha seneti ya chuo kikuu kilichofanyoka February mwaka huu.

Aidha kabla ya uamuzi huo kufikiwa madaktari hao walikumbushwa kurejesha nyaraka hizo za matokeo lakini hawakufanya hivyo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,