ZINAZOVUMA:

Viongozi ECOWAS wakutana kuijadili Niger

Viongozi wa jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi...

Share na:

Wakuu wa nchi wanachama wa jumuia ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) wanakutana katika mji mkuu wa Nigeria Abuja kuanzia leo Jumatano hadi Ijumaa kujadili mapinduzi ya kijeshi nchini Niger.

Siku ya Jumapili, ECOWAS iliiwekea vikwazo Niger na kuonya kuwa inaweza kutumia nguvu huku ikiupa utawala wa kijeshi muda wa wiki moja kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum lakini imeonekana jeshi la Niger limepuuza agizo hilo.

Aidha pia viongozi wa umoja huo unaoongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria Abdulsalami Abubakar unampango wa kufanya ziara nchini Niger ili waweze kutafuta suluhu.

Mapinduzi hayo yamezitia wasiwasi nchi za Magharibi zinazojitahidi kudhibiti uasi wa wanamgambo uliozuka kaskazini mwa Mali mwaka 2012, na kuingia Niger na Burkina Faso na sasa hofu imeongezeka kwa mataifa dhaifu kama vile Guinea.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya