ZINAZOVUMA:

Vifo jengo lililoporomoka Afrika Kusini vyafika 23

Manispaa ya George Afrika Kusini imetangaza kuongezeka kwa vifo vilivyosababishwa...

Share na:

Mamlaka nchini afrika kusini imetangaza kuongezeka kwa idadi ya vifo, vilivyotokana na jengo kuporomoka kutoka 9 hadi 23.

Taarifa ya manispaa ambapo jingo hilo liliporomoka iliendelea kusema kuwa, mbali na ongezeko hilo la vifo 14, pia watu wengine 33 hawajulikani walipo karibu wiki moja tangu kuanguka kwa jingo hilo.

Vikosi vya uokoaji vimekuwa vikifanya kazi bila kuchoka tangu jengo hilo lililokuwa likijengwa kubomka,.

Jengo hilo lilikuwa likijengwa katika mji wa George kusini mwa Afrika Kusini, na lilibomoka Jumatatu alasiri wakati wafanyakazi 81.

Tayari katika juhudi za uokoaji wamefanikiwa kuwaokoa watu 29 hadi sasa.

Siku ya Jumamosi saa takriban 116 tangu kutokea ajali hiyo, aliokolewa manusura kutoka chini ya vifusi vya jengo hilo, ilisema taarifa ya manispaa hiyo.

Jengo hilo lililoporomoka lilitarajiwa kuwa la makazi, na lilikuwa na za makazi ya kutosha familia karibu 41.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya