ZINAZOVUMA:

Upinzani Zimbabwe wataka uchaguzi urudiwe

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe amesema ili suluhu ipatikane basi...

Share na:

Kiongozi wa chama cha upinzani cha CCC nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa jana Jumanne Agosti 29, 2023 amepinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo huku akitaka urudiwe tena.

Chamisa mesema hayo wakati akiongea na vyombo vya habari na kuwataka wananchi wa Zimbabwe kuonesha mshikamano katika kutafuta suluhu la mzozo huu wa kisiasa.

Emmerson Mnangagwa ametetea kiti hicho katika uchaguzi uliofanyika Agosti 23, 2023 kwa ushindi wa asilimia 52.6 dhidi ya asilimia 44 aliyopata Chamisa, huku kukiwa na ukosoaji kutoka kwa waangalizi wa kikanda walioelezea uchaguzi huo kuwa chini ya viwango.

Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ulisema katika ripoti yake Ijumaa kwamba uchaguzi haukufikia takwa la katiba ya Zimbabwe.

Kwa upande wake, Naibu Msemaji wa CCC, Ostallos Siziba amesema ili kuondokana na mzozo uliopo ni vyema uchaguzi urudiwe tena.

“Zimbabwe inahitaji uchaguzi mpya na huru ili kuondokana na mgogoro uliopo,” amesema.

Aidha, Rais Mnangagwa amepinga ukosoaji akisema kwa mara ya kwanza Zimbabwe imeonyesha ukomavu wa kisiasa.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya