ZINAZOVUMA:

UNESCO: Kaburi la Kasubi halipo katika maeneo yaliyo hatarini

UNESCO yakamilisha ukarabati wa Kaburi la kasubi jijini Kampala, ambalo...
Kaburi la Kasubi lililo karabatiwa na UNESCO na Serikali ya Uganda
Picha ya mbele ya Kaburi la Kifalme la Kasubi Jijini Kampala, Uganda.

Share na:

Shirika la UNESCO linalohusika na utambuzi na uhifahi wa maeneo ya kihistoria duniani, limeondoa Kaburi la kifalme la Kasubi kutoka katika orodha ya maeneo yaliyo katika hatari.

Kaburi hilo la kifalme lililopo Jijini Kampala, ni la wafalme wane wa falme ya Baganda nchini Uganda.

Kaburi hilo lililotengenezwa kwa miti na nyasi, liliungua moto mwaka 2010, hali iliyosababisha UNESCO kuliweka katika orodha ya maeneo yaliyo hatarini.

Hatua hiyo ya UNESCO kuitoa katika orodha ya maeneo yaliyo hatarini, ni baada ya juhudi za kukarabati jingo hilo la kihistoria kukamilika.

Ukarabati wa jingo hilo ulifanywa na Serikali ya Uganda pamoja na Shirika la UNESCO, kwa ufadhili wa mashirika mbalimbali duniani.

Ukarabati huo ulioanza mwaka 2013, umekamilika mwaka huu 2023.

Mbali na kurudisha jingo hilo kuwa kama zamani, pia vimewekwa vifaa vya kisasa vya kuzuia moto katika eneo hilo.

Mbali na vifaa hivyo vya kisasa pia wakazi wa eneo hilo la kaburi, wamepewa mafunzo ya uokoaji na kuzima moto kwa ajili ya dharura hiyo.

Viongozi wa Baganda wanaofahamika kama Kabaka, wamezikwa wane katika kaburi hilo.

Viongozi waliozikwa hapo ni Ssekabaka Walugembe Muteesa I (1856–1884), Danieli Mwanga II (1884 – 1888), Daudi Chwa II (1896 – 1939) pamoja na Edward Muteesa II (1939 – 1969).

Miongoni mwa mashirika yaliyo changia ujenzi huo ni, Japanese Fund in Trust, World heritage Fund, Heritage Emergency Fund na Norway Fund.

Mashirika hayo kwa ujumla wake yamechangia zaidi ya Shilingi za Uganda Bilioni 3.5.

Mbali na mashirika hayo kuchangia gharama hizo, Serikali ya Uganda pia imechangia si chini ya Bilioni 2 katika ukarabati huo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya