ZINAZOVUMA:

UN yatilia shaka matokeo ya uchaguzi Zimbabwe

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe ameungana na umoja wa mataifa na...

Share na:

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres ameeleza wasiwasi wake kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Zimbabwe na Rais kutangazwa kushinda.

Hali hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa za kukamatwa kwa waangalizi wa uchaguzi nchini Zimbabwe wakati huo pia kukiwa na madai ya kutishwa na kuhangaishwa kwa wapiga kura.

Aidha kwa upande mwingine kiongozi wa upinzani nchini humo, Nelson Chamisa amepinga kuchaguliwa tena kwa Rais Emmerson Mnangagwa huku akiungana na waangalizi wa kimataifa kuwa uchaguzi haukukidhi viwango vya kidemokrasia.

Tume ya uchaguzi nchini humo ilimtangaza rais Emmerson Mnangagwa mshindi wa uchaguzi huo kwa kupata asilimia 52.6 ya kura zote zilizopigwa.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,