ZINAZOVUMA:

UN yazitaka nchi wanachama kuilinda amani

Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Gutierrez amesema kuwa...

Share na:

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres ametoa mapendekezo ya kukabiliana na kile anachosema ni ongezeko la mivutano ya kisiasa, mizozo na teknolojia zinazokua.

Guterres ameziambia nchi wanachama wa Umoja wa mataifa kuwa vitisho vipya vya leo vinaondoa amani na vinaleta maombi mapya kwetu.

Amesema mapendekezo yake yaliyofafanuliwa katika maelezo mafupi ya sera inayoitwa “Ajenda mpya ya amani,” yanatambua hali ya kuunganishwa kwa changamoto nyingi za kimataifa.

Mizozo imekuwa tete, mibaya na migumu kusuluhisha,” amesema.

Ameongeza kuwa mwaka uliopita ulishuhudia idadi kubwa ya vifo vinavyohusishwa na mizozo katika kipindi cha miongo mitatu.

Amesema Uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine umefanya kuwa vigumu kutatua changamoto nyingi za kimataifa.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya