ZINAZOVUMA:

Makazi ya Israel yanakiuka sheria za kimataifa

Guterres apinga vikali hatua ya Israel kufanya makazi katika ardhi...

Share na:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameitaka serikali ya Israeli kusitisha shughuli zote za ujenzi wa makazi katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa nguvu na Israeli, akaongeza kuwa mpango wao huo utaongeza mvutano na ghasia katika maeneo hayo.

Kauli hii imetolewa baada ya vifo katika kambi ya wakimbizi ya Jenin kilichohusisha pia kijana wa miaka 15, na kuacha majeruhi takriban 90. Vikosi vya Israeli vilivamia kambi hiyo ya wakimbizi na kusababisha mapiganoya muda mrefu dhidi ya wapalestina huko West Bank siku ya Jumatatu.

Guterres alisisitiza kuwa kuweka makazi katika maeneo hayo ya Palestina, uchochezi yanakiuka sheria za kimataifa na yanachochea mahitaji ya kibinadamu, huku yakizidi kuingia katika utawala wa palestina, na kudhoofisha haki halali za Wapalestina kujitawala.

Hivi karibuni, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliidhinisha mipango ya ujenzi wa maelfu ya makazi katika Ukingo wa Magharibi (West Bank) unaokaliwa kwa mabavu, hatua ambayo ilikosolewa na Marekani na kuzua hofu miongoni mwa Wapalestina kuhusu udhibiti wa Israeli katika Ukingo wa Magharibi kwa ujumla.

Ingawa maneno makali ya Guterres dhidi ya Israel yalipokelewa, wachambuzi wanasisitiza umuhimu wa hatua madhubuti kuzingatia kauli hizo pamoja na kuchukuliwa hatua za haraka na wadau wa kimataifa kama Marekani, Umoja wa Ulaya. Na ikitokea hakun ahatua za ziada zitakazochukuliwa basi hata maneno haya ya Guterres yatapuuzwa kama ilivyokuwa hukumu zilizopita juu yao.

Chanzo: Imeboreshwa kutoka Al Jazeera.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya