ZINAZOVUMA:

Ujenzi daraja Dar mpaka Zanzibar wakaribia

Serikali inajiridhisha juu ya teknolojia itakayotumika kujenga daraja kubwa litakalo...

Share na:

SERIKALI imeanza mazungumzo na Kampuni ya China Overseas Engineering Group Company (COVEC) ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa daraja litakalo unganisha Tanzania Bara na Zanzibar.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Godfrey Kasekenya amesema bungeni leo Aprili 28, 2023 kuwa Mazungumzo hayo yameanza Machi 11, 2023 na yalihusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Ujenzi kwa upande wa Tanzania Bara na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa upande wa Zanzibar.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantum Dau Haji aliyetaka kujua mpango wa serikali kujenga daraja hilo, Naibu Waziri Kasekenya amesema bado mazungumzo yanaendelea na serikali inakusudia kujiridhisha na teknolojia zinazotumika katika ujenzi wa madaraja makubwa kabla ya kuanza ujenzi.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,