Ligi kuu nchini Tanzania ‘NBC premium league’ rasmi inaanza hii leo kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja tofauti tofauti huku presha ya kuvuna alama tatu ikiwa kubwa kwa kila timu.
Kila timu inapambana kuhakikisha haipoteze alama wakati wa mwanzo kwani ushindani umeongezeka na kila timu imejipanga kufanya mazuri na zimeboresha vikosi vyao kwa usajili na kuboresha benchi la ufundi.
Timu 16 zinashiriki huku kukiwa na timu tatu zilizopanda daraja msimu huu ambazo ni Tabora United FC, Mashujaa FCpamoja na JKT Tanzania ambazo zote hizi zitapambana kuwania taji la ligi kuu.
Mchezo wa kwanza hii leo utakuwa kwenye Uwanja wa Highland Estates huko Mbarali ambako wenyeji Ihefu wataikaribisha Geita Gold kuanzia saa 10:00 jioni ukifuatiwa na wa saa 12:30 jioni baina ya Namungo dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Majaliwa huko Ruangwa, Lindi na mchezo wa mwisho utakuwa ni baina ya Dodoma Jiji na Coastal Union kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kuanzia saa 3:00 usiku.