ZINAZOVUMA:

Uchaguzi Mkuu Cambodia wa moto

Waziri Mkuu Cambodia atengeneza mserereko uchaguzi mkuu kwa kufungia chama...
Bango la wagombea wa uchaguzi mkuu Cambodia.
Bango la wagombea wa uchaguzi mkuu Cambodia.

Share na:

Nchini Cambodia kumetokea vurumai za chini kwa chini kutokana na figisu za chama tawala katika uchaguzi.

Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika unahusisha vyama 18 nchini humo.

Waziri mkuu wa sasa Hun Sen ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miaka 37 anatarajiwa kupita kwa kishindo baada ya Mahakama ya nchi hiyo kufuta sifa ya ushiriki kwa chama kikuu cha upinzani cha CCP.

Waziri mkuu Hun Sen alishinda uchaguzi wa mwaka 2018 baada ya kukifungia chama kikuu cha upinzani wakati huo cha Cambodia kinachoitwa ‘Cambodia National Rescue Party‘ kisishiriki uchaguzi huo.

Wengi katika wapiga kura wamekuwa wagumu kupiga kura baada ya tukio hilo kujirudia tena mwaka huu.

“Ili mchuano uwe mzuri lazima ulingoni kuwa na wapambanaji wawili, sasa kabaki mmoja kuna haja gani ya kushiriki wakati tunajua matokeo”. Mmoja wa wapiga kura alisema.

Mbali na chama hicho kuzuiwa, pia kumekuwa na hatua mbalimbali za kunyamazisha watu wasiongee chochote kuhusu kufungiwa kwa chama hicho.

Pia tayari watoa huduma za mtandao wamepewa maagizo ya kuzuia baadhi ya tovuti za mashirika ya habari na hata kanzidata mbalimbali za wazi huku vitisho mbalimbali vikiendelea kutolewa.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya