ZINAZOVUMA:

Trump kizimbani kwa kudanganya mali na thamani anazomiliki

Raisi wa zamani wa Marekani Donald Trump ameshtakiwa kwa kudanganya...
Official portrait of President Donald J. Trump, Friday, October 6, 2017. (Official White House photo by Shealah Craighead)

Share na:

Raisi wa zamani wa Marekani Donald Trump anadaiwa kufanya ulaghai wa kutowasilisha kwa usahihi utajiri wake kwa benki na bima, jaji jijini New York alisema katika uamuzi wake.

Uamuzi huo unasisitiza madai muhimu yaliyotolewa na mwanasheria mkuu wa New York katika kesi yake ya madai dhidi ya Rais huyo wa zamani.

“Nyaraka zilizo hapa zina zinadhihirisha wazi ulaghai ambao washtakiwa walitumia katika biashara,” hakimu aliandika.

Hili ni pigo kubwa kwa Donald Trump kabla ya kesi hiyo kusilikizwa Jumatatu ijayo.

Aidha Wakili wa Trump ameutaja uamuzi wa jaji huyo kuwa ni kinyume cha haki na mteja wake ameonewa.

Mwanasheria Mkuu Letitia James alimshtaki Trump Septemba mwaka jana, akimshutumu yeye, wanawe wawili pamoja na Shirika la Trump Organization kwa kudanganya kuhusu thamani na mali zake kati ya 2011 na 2021.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya