ZINAZOVUMA:

TAWA waweka Kambi Mlali kudhibiti mamba

Mamlaka ya uhifadhi wanyamapori nchini TAWA imepiga kambi kijiji cha...

Share na:

Mamlaka ya Uhifadhi na Usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA, imefanikiwa kudhibiti tishio la mamba katika kitongoji cha gudugudu kijiji cha mlali wilayani Mvomero katika mkoa wa Morogoro

Kutokana na changamoto hiyo TAWA imechukua jukumu na kuweka kambi kwenye Kijiji hicho kwa lengo la kuwatafuta mamba ambao wamekuwa tishio kwa wananchi wa kitongoji hicho.

Aidha TAWA wamewaelekeza wananchi namna ya kukabiliana na mamba hao ikiwemo wazazi na walezi kuepuka  kuwatuma watoto kwenye mito pamoja na kuwazuia kuogelea kwani uangalifu wao ni mdogo

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mvomero Judith Nguli amewaasa wananchi kuchukua tahadhari kwenye mito iliyopita kijijini hapo kwani ndio makazi ya mamba yalipo

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya