ZINAZOVUMA:

Tanzania na Marekani kushirikiana kuboresha mifumo ya Afya

Wizara ya Afya chini ya Waziri wake Ummy Mwalimu imeingia...

Share na:

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeingia makubaliano na Serikali ya Marekani juu ya uboreshaji wa mifumo ya usimamizi wa masuala ya Afya kwa kuanzisha Maabara za Taifa za Afya ya Jamii za kisasa.

Makubaliano hayo yamefikiwa mara baada ya Waziri wa Afya Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui kufanya kikao na Mkuu wa Masuala ya Kimataifa Idara ya Afya na Huduma za Kibinadamu nchini Marekani Bi Susan Kim, kwa kujadiliana kuhusu uboreshaji wa mifumo ya usimamizi wa masuala ya Afya.

“Tumekuja hapa kujifunza you jinsi idara hiyo inavyosimamia na kuratibu huduma za maabara za Kitaifa za Afya ya Jamii ambapo tumekubaliana kuanzisha Maabara za Taifa za Afya ya Jamii ambazo zitakuwa na jukumu la ufuatiliaji wa magonjwa hususani yanayoathiri afya ya jamii na vihatarishi vyake, uchunguzi wa magonjwa na tafiti za masuala ya afya ya jamii” amesema Waziri Ummy Mwalimu

Amesema, uanzishwaji wa maabara hizo utaimarisha uwezo wa Tanzania katika kujikinga, kujiandaa na kukabiliana na majanga ya afya kama vile UVIKO 19, Marburg na Ebola.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya