ZINAZOVUMA:

Tanzania ina mazingira rafiki kwa wawekezaji

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape...

Share na:

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye amesema Rais Samia Suluhu Hassan alipomteua kuwa Waziri alimwambia lengo lake ni kuwawezesha Wawekezaji wanaokuja Tanzania kuwekeza bila vikwazo na kufanya kazi zao kwa uhuru.

Waiziri Nape amesema hayo leo Septemba 25, 2023 mkoani Dar es Salaam, wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya Maridhiano na hati wa Mkataba wa nyongeza kwenye Mkongo wa Mawasiliano kati ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Umoja wa Watoa Huduma za Mawasiliano.

Waziri Nape ameongezea kuwa kwa watu wote wanaotaka kuwekeza Tanzania nchi ni salama na Serikali ni rafiki kwao na ipo tayari kujenga mazingira mazuri ili kuhakikisha kuna wawekezaji zaidi.

Aidha, Waziri Nape amesema Serikali imejiandaa vema kutatua matatizo yatakayojitokeza katika uwekezaji na ipo tayari kuyamaliza kwa mazungumzo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,