Sylvia Bongo, mke wa aliyekuwa rais wa Gabon amefungwa kwa matumizi mabaya ya fedha za Umma.
Bi. Sylvia Bongo alikuwa kwenye kifungo cha nyumbani baada tu ya mapinduzi yaliyomtoa mumewe madarakani mwezi Agosti mwaka huu.
Wakili wa Bi. Sylvia amethibitisha kufungwa kwa mteja wake Oktoba 12 2023, na kusema kuwa mchakato wa kesi ya mteja wake haukufuata sheria.
Mtaje wake huyo alikamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya kutakatisha fedha na kughshi nyaraka.
Kama alivyo shitakiwa mke wa Bongo, na mtoto wao Noureddin Bongo ameshitakiwa mwezi
Septemba kwa rushwa na matumizi mabaya ya fedha za Umma.