ZINAZOVUMA:

Sheria dhidi ya uvaaji wa abaya kuanza leo Ufaransa

Mamlaka nchini Ufaransa imeanza rasmi kutekeleza sheria dhidi ya uvaaji...

Share na:

Wiki iliyopita serikali ya Ufaransa ilitangaza marufuku kwa wanafunzi wa kike katika shule za umma kuvaa vazi aina ya abaya ambayo huvaliwa mara nyingi na waumini wa dini ya kiislamu nchini humo.

Hatua hiyo ya kutovaa abaya imekuja baada ya Ufaransa kupiga marufuku alama za kidini katika shule za serikali na hata majengo ya serikali ikisema kuwa zinakiuka sheria za nchi hiyo.

Mapema leo mamlaka nchini humo imesema kuwa inazifuatilia shule takribani 500 mabazo huenda zikakaidi amri hiyo wakati huu shule zinapofunguliwa.

Aidha Rais Emmanuel Macron aliweka wazi kuwa wanafunzi watakaovalia mavazi aina ya abaya au buibui hawataruhusiwa kuingia madarasani.

Alizungumzia kanuni hiyo ya
mavazi kwa mara ya kwanza hadharani baada ya kutembelea shule moja katika eneo la Vaucluse kusini mwa Ufaransa.

Macron amesema anajuwa kutakuwa na visa vya wanafunzi kuijaribu sheria hiyo pamoja na wale watakaojaribu kupinga mfumo huo.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya