ZINAZOVUMA:

Kenyatta na Odinga pamoja kwenye maombolezo

Raisi mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta amejumuika na kiongozi wa...

Share na:

Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria misa ya kuwaombea wananchi wa Kenya waliofariki wakati wa maandamano dhidi ya serikali nchini humo.

Misa hiyo imefanyika leo Ijumaa Julai 28, 2023 katika Kituo cha SKM jijini Nairobi nchini Kenya ambapo ilihudhuriwa pia na Kiongozi wa Azimio Raila Odinga.

Maandamano hayo yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, yalikuwa na lengo la kupinga kupanda kwa gharama za maisha nchini humo, lakini pia kuulalamikia uchaguzi uliopita, ambao ulimuingiza madarakani Rais William Ruto.

Pamoja na Kenyatta, viongozi wengine wa Azimio ambao wamehudhuria misa hiyo ni pamoja na kiongozi wa Azimio Raila Odinga, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na Kiongozi wa kambi ya wachache bungeni, Opiyo Wandayi.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya