Shule nyingi katika mji mkuu wa Manila nchini Ufilipino zilisimamisha masomo ya ana kwa ana siku ya Jumanne kutokana na kiwango cha joto kuwa hatari kwa watu, walisema maafisa wa Elimu.
Kiwango cha hali joto kimetazamiwa kuwa “hatari” cha nyuzi joto 42 katika Mji huo Mkuu siku ya Jumanne na 43 siku ya Jumatano, mtabiri wa hali ya hewa wa serikali alisema.
Utabiri wa halijoto ya juu kabisa kwa Manila Jumanne ulikuwa nyuzijoto 34.
Shule za msingi na sekondari huko Quezon, sehemu yenye watu wengi zaidi ya jiji, ziliamriwa kufungwa huku shule katika maeneo mengine zikipewa chaguo na viongozi wa eneo hilo kuhamia masomo ya mbali.
Baadhi ya shule zilifupisha muda wa masomo ili kuepuka sehemu yenye joto zaidi ya siku.
Inakadiriwa kuwa kiwango cha juu cha joto kuwa kati ya nyuzi joto ya 42C na 51C, na inaweza kusababisha shinikizo la joto, uchovu wa joto na hata kiharusi cha joto ikiwa watu hawatajikinga na hali hii ya joyo kama inavyoendelea, Aliongeza mtabiri kama ushauri kwa wananchi.