ZINAZOVUMA:

ECOWAS yasitisha mpango wa kuivamia Niger

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imesitisha...

Share na:

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imesitisha mpango wake wa kuliingilia kijeshi Taifa la Niger, na kuona badala yake ifanye suluhisho la kidiplomasia.

Awali kulikuwa na mpango wa Jumuiya hiyo kuiingilia kijeshi Niger taarifa zilizokuwa zinaongeza vuguvugu ya uwezekano wa kutokea vita katika ukanda wa Afrika Magharibi.

Kwa mujibu wa tovuti ya The East African, mwishoni mwa wiki, Rais wa Nigeria Bola Tinubu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa ECOWAS, aliashiria kutafuta usuluhishi wa kidiplomasia.

Aidha pia Abdulsalami Abubakar, mjumbe maalum wa ECOWAS kuhusu mkwamo wa kisiasa wa Niger, alitangaza suluhu ya kidiplomasia inaweza kufikiwa kuhusu mzozo ambao umeikumba nchi hiyo.

Abubakar aliwaambia waandishi wa habari kwamba majadiliano na jeshi la nchi hiyo yameonyesha dalili nzuri.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya