ZINAZOVUMA:

Serikali yazindua magari ya umeme Dodoma

naibu Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Doto Biteko amezindua magari...

Share na:

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amezindua magari ya umeme kama jitihada za Serikali kuwezesha wananchi kutumia nishati safi nchini.

Uzinduzi wa magari ya umeme umefanyika jijini Dodoma, sanjari na uzinduzi wa Ofisi za Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na kituo cha kuzalisha umeme wa jua (Solar power Plant).

“Niwapongeze wadau wetu kutoka Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa hatua hii, mtakumbuka kwamba Serikali inaendelea kutafuta mbadala wa kuwawezesha wananchi upata nishati safi, hasa wale walio na uhitaji zaidi wa nishati hiyo”, amesema Dkt. Biteko.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wadau wanaoshirikiana na Serikali kutafuta uwezekano wa kuwa na nishati safi ya uhakika, ili kufikia malengo ya asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ifikapo 2034.

Kwa upande wa Mwakilishi wa UNDP Bi. Weyinmi Omanuli, ameipongeza Serikali kwa hatua zinazoendelea, kuelekea kuwawezesha wananchi wake katika nyanja mbalimbali kijamii na kiuchumi.

Amesema kuwa kampeni ya Nishati Safi ya kupikia imekuwa kielelezo thabiti cha Serikali, kuwajali wananchi wake hususani wale wa kipato cha chini.

Na muwakilishi wa Umoja wa Ulaya Bw. Cedric Marel amesema kuwa, Umoja huo una imani kubwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati, katika kuendeleza jitihada za kuwakomboa wananchi kwa kuandaa mazingira wezeshi yanayolenga kuboresha maisha yao.

“Huu ni mwendelezo wa utekelezaji wa kampeni ya kitaifa chini ya Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inayolenga kuongeza matumizi ya nishati safi nchini” aliongeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika salamu zake za utangulizi.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya