ZINAZOVUMA:

Serikali yawasilisha pingamizi la kulipa Bilioni 267

Serikali ya Tanzania kupitia Mwanasheria wake Mkuu Eliezer Felesh imewasilisha...

Share na:

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Eliezer Feleshi, amesema Serikali imewasilisha maombi ya kuzuia utekelezaji wa hukumu ya Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID), inayotaka Tanzania kulipa Fidia ya Tsh. Bilioni 267.5 kwa kukiuka Mkataba.

Hatua hiyo inafuatia baada ya uamuzi wa ICSID ulioiamuru Tanzania kuilipa kampuni ya Indiana Resources na wadai wengine fidia hiyo kutokana na uamuzi uliofanywa na Serikali ya awamu ya 5 wa kuvunja Mikataba ya Uchimbaji Madini kinyume na Sheria.

Aidha, pingamizi hilo linalenga kulinda Ndege za Serikali ambazo zimeingia hatarini kukamatwa kutokana na uamuzi wa kesi hiyo.

Julai 14, 2023, Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID), kiliiamuru Tanzania kuilipa kampuni ya Indiana Resources na wadai wengine fidia ya kukiuka Mikataba ya Uchimbaji Madini.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya