ZINAZOVUMA:

Serikali ya Mali kuruhusu shughuli za kisiasa

Kiongozi wa Kijeshi na serikali yake waruhusu vyama vya siasa...

Share na:

Tangazo la Serikali ya kijeshi nchini Mali la siku ya Jumatano, limetoa idhini kwa vyama kisiasa kuendeleza shughuli za kisiasa zilizositishwa mwezi Aprili.

“Serikali imeamua kuondoa marufuku ya vyama vya siasa pamoja na shughuli za kisiasa,” imesema taarifa ya baraza la mawaziri, lililosheheni viongozi wa kijeshi waliochukua madaraka katika mapinduzi ya 2020.

Mkuu wa serikali ya kijeshi, Kanali Assimi Goita, alisimamisha shughuli za kisiasa akisema kuwa vyama hivyo vimekuwa vikipotosha umma juu ya mambo ya kitaifa katika shughuli zao za kiasasa.

Vyama hivyo wakati huo vilikuwa vinapinga uamuzi wa kanali wa kubaki madarakani kwa zaidi ya Machi 2024 na kutaka kurejea utawala wa kiraia.

Vyama vya upinzani vilisusia mazungumzo hayoya mwezi mei, yaliyohalalisha uongozi wa kijeshi kubalia madarakani kwa miaka kuanzia miwili hadi mitano.

Pia mazungumzo hayo yalitaka kiongozi wa sasa aruhusiwe kushiriki uchaguzi wowote wa urais nchini humo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya