ZINAZOVUMA:

Serikali kuweka somo la maadili shuleni.

Serikali imesema itaweka somo la maadili katika mtaala wa elimu...

Share na:

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amesema serikali ina lengo la kuingiza somo la maadili kwenye mtaala wa elimu ili kukabiliana na Changamoto ya mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma amesema hayo leo Aprili 18, 2023 Bungeni jijini Dodoma alipokua akijibu swali la Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Viti Maalumu aliyetaka kujua ni lini Serikali italiingiza somo la maadili kwenye mitaala ya elimu.

Mhe. Mwinjuma amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inaendelea kutoa elimu ya maadili na kufanya uhamasishaji wa mabadiliko ya fikra kwenye jamii kupitia vyombo vya habari akibainisha kuwa katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Aprili 2023 wizara imefanya vipindi 11, pia maafisa utamaduni kutoka Halmashauri 16 wamefanya vipindi 21 kwenye vyombo vya habari vya kijamii.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya