ZINAZOVUMA:

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI VISHOKA

Waziri Innocent bashungwa aweka wazi mpango wa Serikali kuwachukulia hatua...

Share na:

“Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika na tuhuma ya kuwa vishoka, kwa kujihusisha na mchezo mchafu wa kushikilia maeneo yenye malighafi za ujenzi” alisema Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25 ya wizara yake, Bungeni jijini Dodoma.

Changamoto kubwa ni uwepo wa vishoka wanaoshikilia maeneo yenye malighafi za ujenzi na kutoza fedha nyingi, alisema waziri Bashungwa.

Wizara ya ujenzi na Wizara ya Madini zinaendelea na mazungumzo, kuhusu upatikanaji wa malighafi za ujenzi ikiwemo changarawe, mchanga na kokoto.

“Mazungumzo hayo yanalenga kupata namna bora ya kutatua changamoto kubwa ya upatikanaji wa malighafi hizo.” amesema Bashungwa

“Dhamira ya Wizara ni kuwa kwa kadri inavyowezekana maeneo hayo yamilikishwe kwa TANROADS, ili kuwezesha miradi mingi ya barabara kutekelezwa kwa wakati na kupunguza gharama za ujenzi.”

Amesema Upatikanaji wa malighafi ya ujenzi kwa gharama nafuu itawezekana iwapo, TANROADS itakuwa na maeneo ya kuchimba madini ya ujenzi na kuondokana na hali ya sasa ya vishoka wanaopandisha gharama za ujenzi kiholela.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana kwenye hotuba yake kupitia mitandao wiki 3

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya