ZINAZOVUMA:

Serikali kuboresha posho ya kujikimu kwa wasimamizi wa Uchaguzi

Mhe. Patrobas Katambi asema kuwa serikali ipo na mpango wa...

Share na:

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema Serikali imefanya maboresho ya viwango vya posho za kujikimu kwa Wasimamizi wa Uchaguzi kuendana na Waraka wa Utumishi wa Umma kuhusiana na posho za serikali.

Amesema hayo hii leo Aprili 22, 2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Angelina Malembeka, ambaye amehoji Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu Mpango wa kuongeza posho kwa Askari na Maafisa Wasimamizi wa Uchaguzi.

Akijibu swali hilo, Mhe. Katambi amesema kuwa wakati wa uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na kata hulipwa posho za kujikimu wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya uchaguzi.

Ameongeza kuwa, kuboresha viwango vya posho ya kujikimu kwa Watendaji na Walinzi wa vituo vya kupigia kura itazingatiwa wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Bajeti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya