ZINAZOVUMA:

Saudi Arabia yataka kujiunga BRICS

Saudi Arabia na nchi nyingne za kiarabu zinazozalisha mafuta zimetuma...

Share na:

Umoja wa nchi zinazozalisha mafuta duniani zimeomba kuungana rasmi na umoja wa nchi za BRICS ambao unaundwa na Brazil, Urusi, India, China pamoja na Afrika Kusini.

Nchi hizo ni Saudi Arabia, Algeria, Egypt, Bahrain, na Iran tayari zimetuma maombi rasmi ya kujiunga na umoja huo ambao unatarajiwa kuwa na kikao hivi karibuni nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Balozi wa Afrika Kusini amesema mpaka sasa zaidi ya nchi 19 zimeonesha nia ya kutaka kujiunga na umoja wa nchi za BRICS ambao ushirikiano wao umejikita katika masuala ya kiuchumi.

Aidha takwimu zinaonesha uchangiaji wa uchumi wa dunia umebadilika kutoka kwa nchi za magharibi ambao ndio walikua wakichangia zaidi na sasa umoja wa BRICS umeonekana kuwa tishio na kuanza kuvutia nchi nyingi zaidi.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya