ZINAZOVUMA:

Saudi Arabia na nchi nyingne kesho Eid.

Saudi Arabia yathibitisha kuonekana kwa mwezi hivyo kesho ijumaa tarehe...

Share na:

Saudi Arabia imetangaza kuwa kesho Ijumaa Aprili 21, 2023 itakuwa Eid El Fitr. Mwezi mchanga unaoashiria mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na mwanzo wa mwezi wa Shawwal umeonekana nchini Saudi Arabia leo Alhamisi jioni.

Kwa mujibu wa Mahakama Kuu ya Saudia, kesho, Ijumaa (Aprili 21), ni siku ya kwanza ya Eid Al Fitr kwa mwaka huu wa 1444 Hijiria.

Aidha kwa upande wa Kamati ya kufuatilia miandamo ya mwezi ya Baraza kuu la Jumuiya ya Ansar Sunnah Tanzania (BASUTA)imewatangazia Waislamu wanaofunga kwa kutazama mwandamo wa mwezi unaoonekana popote ulimwenguni, kwamba mwezi wa Shawwaal (Mfungo wa Mosi) mwaka 1444 Hijiriya umeonekana katika nchi zifuatazo; – Kuwait, Saudia, Bahrain, Qatar, Yemen, Imarati na Palestina.

Kutokana na kuthibiti kwa taarifa hizo za mwandamo wa mwezi sehemu mbalimbali duniani, kesho tarehe 21 April 2023 itakuwa Mwezi mosi (Shawwal) mwaka1444 Hijriya.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,