ZINAZOVUMA:

Saudi Arabia kukuza utalii mpakani mwa Yemen

Saudi Arabia kukuza vituo vya utalii katika eneo la Asir...

Share na:

Serikali ya Falme ya Saudi Arabia imetangaza mpango wa kupanua uwanja wa ndege wa Abha.

Mbali na kupanua uwanja wa ndege, pia mpango huo unajumuisha kufanya eneo la Asir kuwa kivutio cha watalii.

Muhammed Bin Salman (MBS), mwanamfalme wa Saudi Arabia aliweka wazi mpango huo unaotarajiwa kuonngeza yafuatayo.

Mosi, Uwanja huo unachukua ndege 30,000 kwa mwaka, na unatarajiwa kuchukua ndege 90,000 kwa mwaka baada ya upanuzi.

Pili, unatarajiwa kuchukua watu milioni 13, zaidi ya mara nane ya idadi ya sasa ambayo ni watu milioni 1.5.

Tatu, katika upanuzi zitaongezwa huduma mbalimbali kama SPA, njia za kupandia ndege, mifumo ya kuwawezesha abiria kujihudumia “self service” na maegesho ya magari ya kisasa.

Nne, yataongezwa mageti pamoja na madawati ya kuingilia uwanjani hapo.

Uwanja wa Abha upo katika mji wa Asir, karibu kabisa na nchi ya Yemen, na uliwahi kushambuliwa na kundi la Houthi mwaka 2019.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya