Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushuhudia uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Februari leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Uzinduzi wa sanamu hiyo ambayo imesimikwa nje ya Jengo la Amani na Usalama la Mwalimu Julius Nyerere utashuhudiwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na nchi nyingine za AU.
Awali, hoja ya kujengwa kwa sanamu ya Mwalimu Nyerere ilitolewa na Hayati Robert Mugabe mwaka 2017 katika moja ya vikao vya Jumuiya ya SADC na kuungwa mkono na wengi, ambapo maandalizi yalianza hadi kufikia sasa ambapo sanamu hiyo itazinduliwa