ZINAZOVUMA:

Maadhimisho ya miaka 60 Umoja wa Afrika

Leo Afrika inaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa umoja wa...

Share na:

Leo bara la Afrika linaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), unaojulikana sasa kama Umoja wa Afrika (AU), ulioanzishwa rasmi Mei 25, 1963, mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.

AU inaadhimisha Siku hiyo chini ya kauli mbiu ya “Afrika Yetu Mustakabali Wetu” (#OurAfricaOurFuture). Shughuli za kuadhimisha za kihistoria zitafanyika katika bara zima la Afrika na nchi 55 wanachama wa AU.

Nchi zote wanachama zinatarajiwa miongoni mwa mambo mengine kuonyesha mafanikio makubwa, hatua muhimu, changamoto, na njia ya kusonga mbele chini ya Ajenda ya 2063.

AU imesema inaadhimisha Siku ya Afrika, kwa kutambua dira na hatua muhimu iliyofikiwa kuelekea Afrika iliyounganishwa, yenye ustawi na amani, inayoendeshwa na raia wake yenyewe na kuwakilisha nguvu mahiri katika nyanja ya kimataifa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya