Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza, kwani fursa huja na kupotea kwa haraka.
Rais Samia amesema hayo Jana Julai 14, 2023 wakati wa uapisho wa viongozi mbalimbali Ikulu, Dar es Salaam.
“Wakati sisi tunalumbana kuwa bandari apewe nani, iende isiende nani apewe, wenzetu kwa kuona malumbano yetu wamekwenda kulekule na lilelile jumba lilowekwa bendera ya Tanzania limewekwa bendera ya jirani.
“Sasa Tanzania tumesusa sasa jirani wamekwenda kufanya nini? Na siku bunge letu hapa linasema kwamba niruhusu bandari iendeshwe siku ya pili, wenzetu wakasema nyie moja sisi zote zilizopo ziende kwenye sekta binafsi.
“Wenzetu wakakimbia kule kwenda kuwahi nafasi, kama wale wanalumbana njooni huku, sasa muone jinsi fursa zinavyokuja na kukimbia haraka haraka na jinsi wengine wanavyoweza kuzitumia haraka haraka,”amesema Rais Samia.