ZINAZOVUMA:

Ruto atoa onyo maandamano Kenya

Raisi wa Kenya ametoa onyo kali kwa wote wanaopanga kuandamana...

Share na:

Rais William Ruto amevunja ukimya na kutoa onyo kali kuhusu maandamano ya Azimio yaliyopangwa kufanyika siku ya Leo Jumatano.

Akizungumza mjini Ruai, Rais amethibitisha kwamba hataruhusu maisha ya Mkenya yeyote kupotea kutokana na maandamano.

“Walifanya maandamano, na Wakenya wasita wakapoteza maisha yao. Mnataka maandamano ifanyike, maisha mengine yapotezwe? Haitatokea,” Ruto amesema.

Ili kuepuka madhara hayo, Ruto alisema kuwa hataruhusu kifo chochote kutokana na kuridhika au kutoridhika kwa mtu kisiasa.

Kiongozi huyo amewaambia upinzani wanatakiwa kukubali matokeo ya uchaguzi uliofanyika Agosti 2022 kwa maslahi mapana ya Kenya.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya