ZINAZOVUMA:

Ripoti ya C.A.G yaibua makubwa.

CAG aona mengi katika ukaguzi wake mwaka huu. Raisi apendekeza...

Share na:

Raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani amesema ni wazi TTCL imeshindwa kwenye biashara ya mawasiliano ya simu na hivyo anapendekeza ibaki kusimamia makampuni ya simu na mkongo wa Taifa wa mawasiliano.

Raisi Samia ameyasema hayo leo wakati akipokea ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali C.A.G Charles Kichere ikulu Dar es salaam leo tarehe 29 March 2023.

C.A.G Kichere katika ripoti yake aliyomkabidhi Raisi licha ya mambo mengine mengi pia amesema shirika la reli lilimkataa mdhabuni alietaka kulipwa Bilioni 616 na kumpa mdhabuni wa trilioni 1.119 sawa na ongezeko la bilioni 503 lisilokuwa na lazima.

Katika ripoti hiyo pia imegundulika kuwa baadhi ya taasisi za umma zimekusanya mapato nje ya mfumo na hakuna uhakika kama fedha hizo zimeingia serikalini.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya