Wakala wa Nishati Vijijini REA imeshatumia zaidi ya bilioni 70 kufikisha umeme vijiji vya mkoa wa Manyara, kupitia mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa pili.
Katika hatua hiyo wamefanikiwa kufikisha umewe kwenye vijiji takriban 410 katika ya vijiji 440 mkoani humo.
Akiongea katika hafla ya kuwasha vijiji saba kwa mara ya kwanza ndani ya jimbo la mbulu vijijini mkoani Manyara, mkurugenzi mkuu wa Wakala wa huyo wa Nishati Vijijini REA mhandisi Hassan Saidy amesema mpaka ifikapo mwezi wa sita mwaka huu watakuwa wamewasha umeme vijiji vyote 440 vya mkoa wa manyara na kuwataka wananchi kutumia umeme huo kama fursa ya kiuchumi.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mbulu vijijini Flatei Massay amesema umeme utaweza kuwaongezea thamani ya mazao yao kutokana na wananchi wa jimbo lake kutegemea kilimo na ufugaji ikiwemo wa nyuki.