ZINAZOVUMA:

Raisi Ramaphosa ahofia vita na Putin

Ramaphosa ahofia kumkamata Raisi wa Urusi Vladimir Putin, inaweza tafsiriwa...

Share na:

Raisi wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema jaribio lolote la kumkamata Raisi wa Urusi, Vladimir Putin atakapoingia nchini humo litakuwa tangazo la vita na Putin au Urusi kwa ujumla.

Cyril Ramaphosa ametoa onyo hilo zikiwa zimesalia wiki kadhaa kabla ya mkutano wa kimataifa wa nchi za BRICS. Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Johannesburg huku Urusi ni nchi mwanachama, na Putin anatarajiwa kuhudhuria.

Kwa mujibu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, Vladimir Putin atakapotoka nje ya nchi ya Urusi atatakiwa kukamatwa.

Mbali na kuwa Afrika Kusini ilitia saini Mkataba wa ICC, haipo tayari kumkamata kiongozi huyo wa Urusi kwa kile kinachotazamiwa kuwa ni kutangaza vita na Putin au Taifa hilo kubwa la Urusi.

Na hii si mara ya kwanza kwa Afrika Kusini kukiuka agizo kama hilo kutoka ICC.

Mwaka 2017 Afrika Kusini pia, iliwahi kukataa kumkamata Rais wa Sudan wakati huo Omar al-Bashir, ambaye alikuwa akisakwa na ICC kwa uhalifu wa kivita wa mwaka 2015.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya