ZINAZOVUMA:

Rais Tinubu aagiza wauaji wasakwe na jeshi

Rais wa Nigeria Bola Tinubu alaani shambulio la Delta dhidi...

Share na:

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu ameliamrisha jeshi la nchi hiyo kuwasaka na kuwafikisha katika vyombo vya dola waliowaua wanajeshi 16 wa nchi hiyo katika jimbo la Delta kusini mwa nchi hiyo.

Rais Tinubu pia amelaani vikali shambulio hilo lililopelekea vifo hivyo, wakiwemo maafisa wawili wa cheo cha Meja na kapteni mmoja. Aliendelea kusisitiza kuwa shambulio hilo ni hujuma ya moja kwa moja dhidi ya taifa lake.

“Waliotekeleza jinai hii ya kioga na kihaini lazima wawajibishwe na kuadhibiwa,”ameeleza Rais huyo ambaye aliahidi kukabiliana na changamoto za usalama nchini humo tangu alipoingia madarakani.

Vyombo vya Usalama vimepewa ridhaa ya kuhakikisha vikosi vya jeshi la nchi hiyo vinalipa kisasi kwa wahanga wa shambulio hilo katika wanajeshi na raia wa Nigeria.

Bado uchunguzi unaendelea na tayari wametiwa mbaroni watu kadhaa wanaoshukiwa kuhusika na shambulio hilo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya