ZINAZOVUMA:

Bola atangaza hali ya hatari Nigeria

Raisi wa Nigeria Mheshimiwa Bola Tinubu ametangaza hali ya hatari...

Share na:

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ametangaza hali ya hatari kuhusu usalama wa chakula katika juhudi za kukabiliana na mfumuko wa bei ya chakula unaoendelea.

Mikakati ya haraka na muda mrefu imeundwa na serikali ya Nigeria ili kukabiliana na uhaba huo ikiwa ni pamoja na kutoa mbolea na nafaka kwa wakulima kwa kila kaya.

Serikali inapanga kutenga fedha kusaidia sekta ya kilimo na kuanzisha Bodi ya Kitaifa ya Bidhaa ili kudhibiti na kuleta utulivu wa bei za vyakula.

Rais Tinubu amesisitiza malengo na mipango ya kupunguza gharama za chakula ili kukuza kilimo na kuzalisha fursa za ajira.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya