ZINAZOVUMA:

PUTIN AVUNJA HOJA TOKA AFRIKA

Katika hali isiyo ya kawaida Rais Putin amekataa mapendekezo mbalimbali...

Share na:

Katika hali isiyo ya kawaida Rais Putin amekataa mapendekezo mbalimbali ya usuluhishi baina ya Urusi na Ukraine kwa hoja lukuki. Mapendekezo hayo ya usuluhishi yalitolewa na viongozi mbalimbali wa Afrika walipokutana na Raisi huyo anayeheshimika nchini kwake kwa uzalendo na kushutumiwa vikali na mataifa ya magharibi kutokana na vita vinayoendelea baina ya nchi yake na Ukraine.

Pamoja na kukataa mapendekezo hayo alijibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na viongozi hao wa Afrika.

Hoja kubwa ya viongozi wa Afrika ni vita baina ya mataifa hayo yamesababisha uhaba wa chakula duniani huku mataifa ya Afrika, pamoja na kutaka kuona ni namna gani nchi hizo zinaweza kufanya usuluhishi ili kumaliza mzozo uliopo baina yao.

Hata hivyo Rais Putin amesema katika mkutano wake huo na viongozi hao kutoka Afrika kuwa nchi yake iliruhusu kupitisha mazao katika bandari kutoka Ukraine la mataifa ya makubwa yalinunua na kuhodhi mazao hayo hali iliyosababisha kupanda kwa gharama za chakula duniani na haikusababishwa na vita baina ya nchi yake na Ukraine. Pia kuhusu mzozo huo amesema nchi yake haikuwa sababu ya mzozo huo bali Ukraine na washirika wake wa magharibi ndio walioanza chokochoko kabla hata yeye hajaingiza vikosi vyake nchini Ukraine. Na kuongezea kuwa Urusi haikukata mawasiliano na Ukraine bali Ukraine ndio haitaki mazungumzo baina yao.

Viongozi hao waliokutana na Rais siku ya Jumamosi, pia walikutana na raisi wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy siku kabla Mjini Kyiv. Na raisi wa Ukraine alisisitiza kuwa hawezi kukubali mazungumzo na Urusi hadi atakapotoa vikosi vyake katika ardhi ya Ukraine anayokalia kimabavu.

Viongozi hao waliokutana na Rais siku ya Jumamosi, pia walikutana na raisi wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy siku kabla Mjini Kyiv. Na raisi wa Ukraine alisisitiza kuwa hawezi kukubali mazungumzo na Urusi hadi atakapotoa vikosi vyake katika ardhi ya Ukraine anayokalia kimabavu.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya