ZINAZOVUMA:

Polisi: Watano wafariki kwa kuchomwa kisu jijini Sydney

Polisi jijini Sydney imetoa taarifa ya vifo vya watu watano...
Police cordon off the Westfield Bondi Junction shopping mall after a stabbling incident in Sydney on April 13, 2024. Australian police on April 13 said they had received reports that "multiple people" were stabbed at a busy shopping centre in Sydney. (Photo by DAVID GRAY / AFP)

Share na:

Polisi mjini Sydney nchini Australia wamethibitisha kuwa watu watano wamefariki, na wengine kadhaa wamepelekwa hospitali katika hali mbaya. Hiyo ni baada ya watu hao kushambuliwa na mwanaume wa makamu kwa kisu katika maduka ya Westfield jijini humo.

Watu zaidi ya tisa wanaamiwa kushambuliwa kwa kisu na mshukiwa huyo, polisi inasema.

Katika mazungumzo na waandishi wa habari muda mfupi uliopita, walisema kuwa mshukiwa “aliwavamia takriban watu tisa” alipokuwa akipita katikati ya maeneo ya hayo ya maduka.

” alisababisha madhara kwa watu hao, tunaamini kwa kuwachoma na silaha aliyokuwa amebeba,” kamishna msaidizi Anthony Cooke alisema.

Miongoni mwa waliojeruhia ni mtoto mdogo na yupo hospitali anaendelea na matibabu, afisa huyo anathibitisha.

Mshambuliaji ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi wa kike aliyemfuatilia kwa ushujaa silaha katia sakata hilo.

Kutokana na shambulizi hilo kulikuwa na taharuki kubwa kwa wateja wengine waliopo maeneo hayo., na kusababisha watu kuonekana wakikimbia huku na huko.

Vyombo vya habari vimeonyesha uwepo wa magari ya kubebea wagonjwa na pamoja na polisi wengi kwenye eneo hilo la tukio.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya