ZINAZOVUMA:

OPEC+ kupunguza uzalishaji mafuta.

Muungano wa OPEC umepanga kupunguza uzalishaji wa mafuta hali itakayotishia...

Share na:

Muungano wa OPEC + umepanga kupunguza uzalishaji wa mafuta ili kudhibiti bei ya bidhaa hiyo muhimu duniani.

Muungano huo ukiongozwa na Saudi Arabia utapunguza kiasi cha Mapipa Milioni 1.5 kila siku kuanzia Mei 2023 huku ukiita hatua hiyo ni ya tahadhari na inayolenga utulivu wa soko.

Kupunguza kwa uzalishaji pekee kunaweza kupandisha bei ya petrol kwa marekani kwa zaidi ya senti 26 kwa galoni, pamoja na ongezeko la kawaida ambalo hutokana na gharama za usafirishaji.

Ikumbukwe kuwa, Oktoba 2022 Nchi za OPEC+ zilikubaliana kupunguza uzalisha wa Mafuta kwa Pipa Milioni 2 kwa siku, hatua iliyoikasirisha Marekani kwa maelezo kuwa itasababisha Mfumuko wa Bei duniani kote.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya