ZINAZOVUMA:

Odinga atumia ‘Matatu’ kwenda kazini

Kiongozi wa Azimio la umoja nchini Kenya Raila Odinga ametumia...

Share na:

Kiongozi wa Azimio la Umoja nchini Kenya, Raila Odinga mapema leo Jumatatu, Julai 10, 2023 ametumia usafiri wa umma maarufu matatu nchini humo wakati akienda kazini.

Kabla na baada ya kupanda kwenye matatu, Odinga amesalimia na abiria wenzake na wengine wakionekana kumshangaa na kuzungumzana naye maneno mbalimbali.

“Nikiwa kwenye usafiri rahisi na rafiki wa umma nikielekea kazini asubuhi ya leo,” ameandika Odinga.

Ndani ya usafiri huo uliokuwa ukipitia barabara ya Ngong-Nairobi, wapiga debe wakilalamikia gharama ya juu ya mafuta.

Abiria wengine walimweleza kuhusu gharama ya juu ya maisha, wakisema nchi haiendi kwenye mwelekeo sahihi.

Hata hivyo hali bado si shwali nchini Kenya baada ya vifo vya watu vilivyotokana na maandamano ya kupinga kuongezeka kwa kodi kufikia watu wa tatu mpaka hivi sasa.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya